DAR-Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini na pia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Manyara kwa nyakati tofauti Dkt.Derick Magoma amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu, Dkt.Magoma amefariki Februari 9,2025 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Dkt.Magoma wakati wa uhai wake anatajwa kuwa alikuwa ni kijana mcheshi, mnyenyekevu na mtu aliyependwa sana na jamii.
Pamoja na kwamba alikuwa kiongozi, mwanasiasa aliyekipenda na kukitumikia chama chake hasa, hakuwahi kuwa na mgogoro wowote na mtu yeyote kwa itikadi ya vyama.
Dkt.Magoma pia katika harakati zake pia hakuwahi kuwa na mgogoro na dola,alipendwa na wengi na kuchukiwa na wachache.