Dkt.Mpango awasili nchini Namibia

WINDHOEK-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango tarehe 27 Februari 2025 amewasili Jijini Windhoek nchini Namibia ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Namibia hayati Dkt. Sam Nujoma.
Utoaji wa heshima za mwisho na Ibada ya kumuaga Kitaifa hayati Dkt. Nujoma itafanyika katika Uwanja wa Michezo wa Uhuru uliopo Jijini Windhoek tarehe 28 Februari 2025 na Mazishi yatafanyika katika eneo la Makaburi ya Mashujaa yaliyopo katika Jiji la Windhoek nchini Namibia tarehe 01 Machi 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news