DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasili Dodoma kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 48 ya Kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Dkt.Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Mohamed Said Dimwa.