DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameongoza kikao cha Serikali na Ujumbe kutoka Kampuni ya Leonardo ya nchini Italia, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika, Bw. Claudio Sabatino, ambapo wamejadili namna Kampuni hiyo inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Madeni, Bw. Omary Khama, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine wa Serikali na Kampuni ya Leonardo.