WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika Treni ya Kisasa (SGR) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia ambaye pia anaziwakilisha nchi za Zambia, Malawi na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete, wakiwahi kushiriki Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo unaotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Treasury Square jijini Dodoma.

Mradi wa SGR ambao kipande cha kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kimekamikika, ni miongoni mwa miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali na umepata uungwaji mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia na umekuwa Mradi maarufu unatumiwa na watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali.