Elimu ya fedha yawafikia wananchi Kata ya Makanya wilayani Same

NA CHEDAIWE MSUYA
WF Kilimanjaro

WANANCHI wa Kata ya Makanya, Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro, wameipongeza Serikali kwa kuwapelekea elimu ya fedha ambayo inatarajia kuwa kichocheo cha maendeleo yao ya kiuchumi.
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaj wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha na vile vya kijamii kwa wananchi wa Kata ya Makanya, kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa kwa wananchi hao katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Mafunzo hayo yamelenga wananchi, wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima, wafugaji, watumishi wa Umma na Binafsi, Watoa Huduma za Fedha ili kufahamua Sheria, Kanuni na Miongozo ya Huduma Ndogo za Fedha na kufahamu masuala ya Akiba, Mikopo, Uwekezaji wa Fedha, Bima, Matumizi bora ya Fedha na kujipanga na maisha ya baadae/uzeeni.
Baadhi ya wajasiriamali na wananchi pamoja na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Makanya, Wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, alieleza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha, ikiwemo kupanga bajeti, kuweka akiba, na mikopo salama.

“Matatizo mengi ya kifamilia hutokana na changamoto za kifedha, hivyo elimu hii itasaidia kuboresha maisha ya familia nyingi, na ndoa nyingi zinazovunjika hutokana na mzigo wa madeni. Nahimiza ushirikiano kati ya wanandoa katika kupanga matumizi ya mikopo,"alisema Bi. Dionesia.
Diwani wa Kata ya Makanya, Mhe. Damari Kangalu, akichangia mada zilizotolewa na Timu ya Wataalam, Kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Diwani wa Kata ya Makanya, Mhe. Damari Kangalu alitoa shukrani kwa Wizara ya Fedha kwa kuwapelekea mafunzo hayo muhimu kwa wananchi wake na kwamba elimu hiyo itawasaidia wananchi kuepuka mikopo umiza na kuimarisha hali yao ya kifedha.

“Hata wale wenye kipato kidogo wanaweza kuweka akiba na hatimaye kuwekeza ili kupata faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Hili litasaidia kuinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla,”alisema Bw. Kangalu.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya akifafanua kuhusu masuala ya mikopo salama na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, alieleza kuwa Wapo Watoa huduma za fedha wasio waaminifu na hawatoa taarifa sahihi za huduma zao kwa wateja hali hiyo imesababisha watumiaji wengi kutojua wajibu wao na kusababisha migogoro kati yao, hivyo kila Mtoa huduma ahakikishe kabla ya kutoa huduma wanatoa elimu ya fedha nakuweka wazi wajibu wa Mtoa Huduma na Mteja kwenye mkopo au huduma anayotoa.
Afisa Ushirika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Bw. Adolf Felix Ndunguru, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa Mkuu kutoka Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Mwile kauzeni akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Mratibu wa huduma ndogo za fedha same DC, Bw. Ally Msumi, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa wa Uendeshaji wa Mfuko Wa Uwekezaji Wa Pamoja Wa Wekeza Maisha (UTT AMIS) Tawi la Arusha, Bw. Elias Nyakimura Muhoji akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Wananchi wa Kata ya Makanya walieleza kufurahishwa na mafunzo hayo yanayotolewa na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake kwa kuratibu elimu hiyo muhimu.

Mafunzo hayo yanatolewa katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro, zikiwemo Wilaya ya Same, Mwanga, na Rombo.
Baadhi ya wajasiriamali na wananchi pamoja na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Makanya, Kata ya Makanya, Wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wakichangia mada mbalimbali kuhusu elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Same).

Kupitia juhudi hizo, wananchi wengi zaidi wataweza kutumia fedha zao kwa ufanisi, kujikwamua kiuchumi, na kujenga maisha bora kwa siku za usoni.

Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha ilitoa elimu kwa washiriki zaidi ya 700 juu ya usimamizi wa fedha, mbinu za uwekezaji, na umuhimu wa kuweka akiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news