Eneo la Dakawa kutangazwa Urithi wa Taifa

MOROGORO-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa eneo la kihistoria la Dakawa lililopo wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro lipo kwenye hatua ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali kuwa miongoni mwa Urithi wa Taifa kisheria.
Waziri kabudi ameyasema hayo Februari 08, 2025 wakati wa ziara yake katika eneo la kihistoria la Dakawa mkoani Morogoro, ambapo ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza Utalii wa Ukombozi wa Afrika nchini.

Aidha, Waziri Kabudi amekitaka Kituo cha Urithi na Ukombozi wa Afrika kilichopo chini ya Wizara yake kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Wizara ya Elimu, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kuratibu uendelezaji wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu iliyopo.
Katika hatua nyingine, Prof. Kabudi ametoa zawadi kwa Mwalimu na mwanafunzi aliefanya vizuri kwenye somo la Historia katika shule ya sekondari Dakawa na kusisitiza kujengwa Kituo cha taarifa za kumbukumbu za historia ili kuwapa fursa wanafunzi kupata maarifa ya historia hii adhimu.

Eneo hili la kihistoria la Dakawa lilitumika kuratibu harakati za ukombozi wa Afrika ya Kusini zilizoongozwa na Oliver Tambo kuanzia mwaka 1982 hadi 1992 baada ya hali ya kisiasa nchini humo kuimarika na wapiganaji hao kurudi nchini kwao na kurejesha eneo hilo kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama sehemu ya kumbukumbu ya historia ya Ukombozi wa Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news