Halmashauri ya Chamwino yapongezwa kwa usimamizi wa miradi

DODOMA-Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeipongeza Halmashauri ya Chamwino kwa kuonesha na kusimamia thamani ya fedha katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya elimu katika halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justin Nyamoga ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya elimu ambapo Kamati hiyo ilitembelea katika Shule ya Sekondari Wasichana Manchali na Shule ya Msingi Membe.
“Ukipita utaona thamani ya fedha inaonekana katika miradi hii, fedha iliyoletwa inaendana na matokeo tunayoyaona kwa hiyo Kamati inawapongeza wote Kwa usimamizi mzuri wa miradi.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Festo Dugange, amesema ofisi yake imepokea maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Kamati hiyo na kuyasimamia katika Halmashauri mbalimbali Nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news