TANGA-"Kwa miaka 15 sasa, wananchi wa Jimbo la Bumbuli tumekuwa tukihadaiwa na ahadi zisizotekelezeka. Tumeshuhudia mbunge wa msimu, anayejitokeza tu nyakati za uchaguzi kama mtalii, kisha kutoweka bila kutatua matatizo yetu ya msingi. Leo, kwa umoja wetu, tunasema January Makamba IMETOSHA!.
"Jimbo letu limebaki nyuma kimaendeleo, huku wananchi wakikosa huduma muhimu kama maji safi, barabara za uhakika, huduma bora za afya, na fursa za kiuchumi.
"Tumechoka na tunasema hatutamchagua tena January Makamba. Tunamtaka apumzike, na tunatoa wito kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutusikiliza, kwani sauti ya wananchi ni sauti ya Mungu.
"Wananchi wa kata zote 18 za Jimbo la Bumbuli kwa kauli moja tunasema:
1. Baga
2. Bumbuli
3. Dule "B"
4. Funta
5. Kisiwani
6. Kwemkomole
7. Mahezangulu
8. Mamba
9. Mayo
10. Mbuzii
11. Mgwashi
12. Milingano
13. Mponde
14. Nkongoi
15. Soni
16. Tamota
17. Usambara
18. Vuga
"Tumesema kwa kauli moja, January Makamba hatufai tena! CCM isituangushe kwa kupuuza sauti yetu. Yeyote atakayepuuza ujumbe huu ataanguka ANGUKO KUU."
Tags
Habari