JKCI yarejesha tabasamu kwa wagonjwa wa moyo ndani na nje ya nchi

DODOMA-Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema toka huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Dkt.Samia Suluhu Hassan Outreach Services ianze imeshawafikia watu 21,324.

Kati ya hao watu wazima wakiwa 20,112 na watoto 1,212 katika mikoa 20 nchini waliofanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na wagonjwa wengine 689 walitibiwa kutoka nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt.Peter Kisenge ameyasema hayo Februari 26,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maendeleo ya hospitali katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Kisengi amefafanua kuwa,kati ya hao 8,873 watu wazima wakiwa 8,380 na watoto 493 walikutwa na matatizo mbalimbali ya moyo na kuanzishiwa matibabu.

“Wagonjwa 3,249 watu wazima 2,765 na watoto 484 walikutwa na matatizo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika taasisi yetu.

“Wagonjwa hao walitoka katika nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Comoro , Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbabwe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia, Burundi na wengine kutoka nje ya Afrika zikiwemo nchi za Armenia, China, Ujerumani, India, Norway, Ufaransa na Uingereza.

“Wataalamu wetu walivuka mipaka ya nchi na kwenda kutoa huduma za matibabu ya moyo katika nchi za Malawi, Zambia na Jamhuri ya Watu wa Comoro wakiwa katika nchi hizo walitibu wagonjwa 1,189 watu wazima walikuwa 851 na watoto 338. Wagonjwa 262 walipewa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI."

“Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua na kubadilishwa Valvu za moyo moja hadi tatu, upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery-CABG), upasuaji wa mishipa ya damu na mapafu walikuwa 2,784 kati ya hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news