DAR-Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu kwa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi, aliyoadhibiwa na mwamuzi wa mchezo wa Namungo FC dhidi ya Simba SC.
Kamati imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo.
Aidha, mchezaji wa Namungo, Daniel Amoah ameadhibiwa kwa kutozwa faini ya shilingi 500,000, kwa kosa la kuonekana akimwaga vimiminika kwenye goli, jambo lililohusianishwa na vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina.