JAMHURI ya Kidemokrasi ya Congo imetoa wito Rwanda iwekewe vikwazo na kupunguzwa kwa misaada na pia isimamishwe ushiriki wake katika misheni ya kulinda amani ya UN kwa jukumu ambalo inadaiwa kutekeleza katika mzozo wa Congo Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo DR, Therese Kayikwamba aliiambia BBC, Rwanda inakalia eneo la nchi yake kinyume cha sheria.
Therese amesema Rwanda inaunga mkono, kufadhili na kuandaa ujasusi ambao unatafuta kupindua serikali iliyochaguliwa kisheria.
Wakijibu suala hilo, Msemaji wa Serikali ya Rwanda Yolande Makolo amesema nchi yake inatetea mipaka yake wala haina nia ya mabadiliko ya serikali.
Viongozi wa waasi ambao walichukua udhibiti wa baadhi ya sehemu za Jiji la Goma wiki hii walisema Alhamisi kwamba wanakusudia kufika Kinshasa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo