DAR-Rais wa Jamhuri ya Cabo Verde, Mhe. José Maria Pereira Neves amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu katika Ufunguzi wa Mwaka 2025 wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu utakaofanyika Februari 3, 2025 jijini Arusha.
Rais Neves amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa.
Kabla ya kuingia madarakani, Rais Neves aliwahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu wa Cabo Verde kwa miaka 15.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo