SHARJAH-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameendelea na ziara yake nchini Sharjah kwa kutembelea Kituo cha Ulinzi wa Watoto cha Kanaf.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi amefahamishwa kuhusu huduma za kituo hicho ikiwa ni pamoja na msaada wa haraka wa kisheria, kisaikolojia na jamii kwa waathirika wa unyanyasaji wa watoto.
Vilevile Mama Mariam Mwinyi ametembelea Baraza la Sanaa la Kisasa la IRTH (ICCC) mpango unaolenga kuhifadhi urithi na utamaduni wa Emarati kwa kuunganisha ufundi wa jadi na ubunifu wa kisasa.
Mama Mariam Mwinyi amepongeza mpango huo kama mfano mzuri wa uwezeshaji, urithi na ufundi.
Pia ametembelea Sharjah Children, Shirika Tanzu la RubiQam Foundation for Creating Leaders and Innovators.
Kituo hicho kina jukumu la kukuza maendeleo ya ujuzi,kuimarisha utambulisho wa Taifa na maadili ya pamoja.