ADDIS ABABA-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi, ameshiriki katika Mkutano wa 29 wa Kawaida wa Taasisi ya Maendeleo ya Wake wa Marais wa Afrika (OAFLAD) ulioshirikisha pamoja na Wake wa Marais kutoka mataifa 17 barani Afrika, katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa Ethiopia.
Mkutano huu unalenga kuzindua Mpango Mkakati wa OAFLAD wa mwaka 2025-2030, ambao unazingatia sekta za afya, elimu, uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Vilevile , mkutano huo unahusisha uchaguzi wa Rais mpya wa OAFLAD kufuatia kumalizika kwa muda wa Rais wa sasa.