ADDIS ABABA-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa Nchini Ethiopia leo Februari 14, 2025.
Katika Uwanja wa Kimataifa nchini humo alipokelewa na Viongozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje Ethiopia Balozi, Dkt. Aziza Gelete.