Mawakala wa Sekta ya Milki watakiwa kujisajili

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM Arusha

MAWAKALA wa Milki nchini wametakiwa kujisajili katika mfumo wa Wizara ya Ardhi ili kuingia kwenye mfumo rasmi utakaowezesha kutambulika.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Wilson Wairara akizungumza wakati wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Hayo yameelezwa leo Februari 12,2025 na Mratibu wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa Wadau wa Sekta ya Milki, Bi. Nuru Kimbe, mjadala uliofanyika mkoani Arusha.

Amesema, ni vizuri mawakala wa milki wakajisajili katika mfumo ili waweze kutambulika katika kipindi hiki ambacho wizara inategemea kuwa na sheria ya milki.
Sehemu ya washiriki wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki wakifuatilia uwasilishwaji mada wakati wa mjadala uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.
Bw. Bariki Ileta kutoka Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwasilisha mada kwenye Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

"Nasisitiza mawakala waweze kujisajili na waweke ‘details’ za masingi kama anuani na mahali wanapofanyia kazi,"amesema Bi.Nuru.

Kwa mujibu wa Bi. Kimbe ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, faida za kujisajili ni pamoja na kutambulika na serikali kitu alichokieleza kitarahisisha kazi kwa mawakala ambapo amesema hatua hiyo itarahisisha katika kazi zao kama wakala na kuwafikia wateja sambamba na kuaminika zaidi.

Amebainisha kuwa, kwa sasa mijadala inafanyika kwenye majiji ambako soko la milki linafanyika sana na kuitaja majiji hayo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza.

Hata hivyo, amesema wako katika mchakato wa kufika mikoa mingine inayokuwa sana katika soko la milki kama vile Tanga, Morogoro, Pwani na Mbeya huku nia ikiwa ni kufika nchi nzima.
Mwakilishi wa kampuni ya GimcoAfrika Ltd Bw.Herien Muro akichangia mada wakati wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.
Bw. Gerald Mboya kutoka kampuni ya Arusha Homes akichangia mada wakati wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa kikao hicho kutoka kampuni ya GimcoAfrika Ltd Bw. Herien Muro amesema, elimu waliyopata kupitia kikao kazj ni muhimu kwa kuwa inaenda kuondoa udanganyifu huku ikiisaidia serikali kupata mapato.
Washiriki wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mjadala uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kitengo cha Milki (REAL ESTATE) inaendesha mijadala ya pamoja na wadau kwa lengo la kupata maoni kuhusu utambuzi na usajili wa wadau wa sekta ya milki ili kuboresha na kukuza sekta ya milki nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news