DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wamekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, anayeziwakilisha pia nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete, katika Ofisi za Wizara ya Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuongeza ushirikiano katika kuendeleza biashara na uwekezaji kwa kushirikiana na Sekta Binafsi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, anayeshughulikia Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda Ezekiel na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango na Maafisa wengine waandamizi kutoka serikalini.