DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wamekutana na kufanya mazungumzo na Wenyeviti Wenza wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo wakiongozwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali kuelekea Mkutano wao, utakaofanyika tarehe 28 Februari 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage, Treasury Square jijini Dodoma.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Mwenyekiti mwingine Mwenza wa Washirika wa Maendeleo, Bi. Susan Ngongi Namondo na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha, Tume ya Mipango na Maafisa wengine waandamizi kutoka serikalini na Ofisi ya Washirika wa Maendeleo.