DODOMA-Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Mheshimiwa Anthony Mavunde amekabidhi mradi wa shamba la zabibu kwa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA).
Huo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano kubwa la wafanyabiashara wanawake wa masokoni wakati wa mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa UWT, Mary Chatanda.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Februari 20,2025 Mpunguzi jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wanachama wa UWAWAMA.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko jijini Dodoma, kazi ambayo imechochea kukua kwa biashara na kuongezeka kwa kipato kwa wafanyabiashara wadogo.
"Mradi huu wa shamba la zabibu unategemewa kuongeza mapato na kutunisha mfuko wa wafanyabiashara wadogo.
"Ni imani yangu kwamba mradi huu wa shamba utakuwa kichochea cha kukua kwa uchumi na mapato ya Umoja na kuongeza tija kubwa katika biashara zenu na nitahakikisha mnapata soko la uhakika wa mazao yenu.

Naye Mwenyekiti wa UWAWAMA,Bi. Anna James Mwita amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo anavyowajali wakinamama na kuwainua kiuchumi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kuutunza na kuuendeleza mradi huo.
Lengo ni ili ulete tija kwa wakinamama wa masokoni sambamba na matumizi yenye tija ya fedha shilingi milioni 10 kwa lengo la kutunisha mfuko wa umoja.