Mchimbaji mdogo wa dhahabu ampa tano Rais Dkt.Samia, vijana watakiwa kuwa waaminifu

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanapata mitaji, leseni na matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuwezesha kuchimba kisasa.
Akizungumza katika mahojiano maalum mmiliki wa Mgodi wa Kwasakwasa uliopo kijiji cha Msesule kata ya Mapogoro, wilayani Mbarali mkoani Mbeya, mwanadada Amagite Mkumbwike amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mazingira wezeshi ikiwemo bei nzuri sokoni ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika zaidi.

“Nikiwa mchimbaji mdogo na mmiliki wa mgodi wa Kwasakwasa, nitaendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana na kurudisha faida kwa kile kinachopatikana katika vijiji vinavyozunguka mgodi wetu,”amesema na kuongeza,
“Serikali imerahisisha vitu vingi ikiwemo kuhakikisha bei ya dhahabu sokoni zinakuwa juu ili wachimbaji wadogo tunufaike. Tumeendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kurudisha faida kwa jamii ikiwemo kununua vifaa vya shule kwa wanafunzi wa kijiji hiki ambao wameendelea na masomo yao ya elimu ya juu, pamoja na kununua mashine ya umwagiliaji hapa kijijini,”amesema Amagite

Aidha, kwa upande wa Msimamizi wa Mgodi huo Edward Daud ameiomba Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji ili vijana wengi wapate ajira kutokana na uwekezaji unaofanywa.

“Na sisi vijana tunapoaminiwa sehemu yoyote ile tukapewa kazi basi tuifanye kwa bidii kwa asilimia 100, tuwe waaminifu kwa waliotupa dhamana,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news