Mchungaji Godfrey Malisa afukuzwa CCM

KILIMANJARO-Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.
Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema, uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na ubunge alijiunga na CCM mwaka 2021 na pia alikuwa mmoja wa makada tisa waliochukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho mwaka 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news