MOROGORO-Ofisi ya Rais-TAMISEMI imezielekeza ofisi za wakuu wa mikoa kote nchini kuhakikisha kuwa rasimu za mikataba ya huduma kwa mteja zinawasilishwa ifikapo Februari 20, 2025.
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Miundo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Peter Mhimba (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo hayo mjini Morogoro yaliyotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Rasimu hizo zitafanyiwa maboresho kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa ajili ya idhini ya matumizi rasmi, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Miundo, Peter Mhimba ameyasema hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, alipokuwa akifunga mafunzo ya uandaaji wa mikataba ya huduma kwa mteja kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Utawala na Rasilimaliwatu pamoja na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutoka ofisi za wakuu wa mikoa yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Miundo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Peter Mhimba akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja (hawapo pichani) kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakati akifunga mafunzo hayo mjini Morogoro yaliyotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa Miundo, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Peter Mhimba akifunga mafunzo hayo mjini Morogoro, yaliyotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Mkufunzi wa Mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Noah Mkasanga akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo, yaliyotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-UTUMISHI katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa mteja kutoka ofisi za wakuu wa mikoa, wakimsikiliza Mkufunzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Noah Mkasanga (hayupo pichani) wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo yaliyotolewa mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
"Tunahitaji kuona rasimu hizi zikifikishwa TAMISEMI kwa wakati ili zifanyiwe maboresho kabla ya kuwasilishwa kwa UTUMISHI ifikapo Machi 31, 2025 kwa ajili ya idhini rasmi," amesisitiza Mhimba.
Aidha, amewasihi viongozi wa sekretarieti za mikoa kuhakikisha mikataba hiyo haikai kwenye makabati mara tu inapokamilika, bali izinduliwe rasmi na kuwafahamisha wananchi kuhusu umuhimu wake katika kuboresha huduma za serikali.
Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Emmanuel Kayuni akiahidi kutekeleza maelekezo ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, mara baada ya Mkurugenzi wa Miundo Bw. Peter Mhimba kufunga mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa viongozi wa ofisi za wakuu wa mikoa yaliyotolewa katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Kwa niaba ya Makatibu Tawala, Emmanuel Kayuni ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mbeya, ameahidi kutekeleza maelekezo hayo kwa wakati na kuhakikisha mikataba inawasilishwa kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Bi. Khadija Dalasia, akiahidi kutekeleza maelekezo ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, mara baada ya Mkurugenzi wa Miundo Bw. Peter Mhimba kufunga mafunzo ya uandaaji wa mkataba wa huduma kwa viongozi wa ofisi za wakuu wa mikoa yaliyotolewa katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Khadija Dalasia, ameahidi kuwa watahakikisha wananchi na wadau wote wanapata taarifa kuhusu mkataba huo kupitia tovuti, mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, na nakala zilizochapishwa.
Mafunzo hayo ya siku nne yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa lengo la kuhakikisha kila mkoa unaandaa na kutekeleza mkataba wa huduma kwa mteja kwa ufanisi.