Miradi yote ngazi ya msingi itangazwe kupitia NeST

DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa Nest.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi kuhusu mfumo wa Nest kilichofanyika kwenye ukumbi wa wa Mabeyo jijini Dodoma Februari 4,2024.

Amesema baada kupata mafunzo haya leo hii nendeni mkabadilike, fuateni Sheria ya Manunuzi, onyesheni mabadiliko hayo kwenye utekelezaji wa miradi na kuanzia sasa miradi yote itangazwe kupitia mfumo wa Nest na si vinginevyo alisisitiza.

Miradi hiyo ikishatangazwa kupitia Nest hakikisheni mnaisimamia kwa Weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha iweze kuonekana’ amesema!

Aidha Mhe. Mchengerwa aliwataka PPRA kuhakikisha inawajengewa uwezo watumiaji wa mfumo wa Nest katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kuomba zabuni mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news