PWANI-Kivuko cha Mv Kilindoni kinachotoa huduma kati ya Mafia wilayani Mafia na Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani kitasimama kutoa huduma katika eneo hilo kuanzia Februari 12, 2025 ili kupisha matengenezo pamoja na kufungwa injini mpya.
Kivuko cha Mv Kilindoni kiliwasili kikiwa na abiria pamoja na mizigo eneo la Nyamisati kikitokea eilayani Mafia.
Kivuko hicho kinapelekwa mkoani Dar es Salaam ambako kitakuwa huko kwa muda wa wiki moja kikifanyiwa matengenezo hayo ili kukiongezea ufanisi kiweze kurejea kikiwa bora na salama kwa watumiaji.
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umewaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu watakaoupata kutokana na kukosekana kwa huduma ya kivuko hicho.