Naibu Waziri Chumi afanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Brunei jijini Muscat

MUSCAT-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (Mb.) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bal. Mohamoud T. Kombo (Mb.) amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brunei Mhe. Erywan Yusof jijini Muscat, Oman.
Wakati wa mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana ili kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Brunei.

Viongozi hao pia wamekubaliana kuanzisha majadiliano yayakayotoa Mkataba wa Ushirikiano katika masuala mbalimbali; kama vile kuwa na Wawakilishi wa Heshima (Honorary Consul) kati ya Tanzania na Brunei na kuhimiza wananchi wa nchi hizo kutembeleana, kufanya biashara, kutalii na kuwekeza ili kunufaika na fursa zilizopo katika nchi hizo.
Katika tukio lingine, Mhe. Chumi alikutana na kuzungumza na Mshauri wa Mfalme wa Oman wa Masuala ya Biashara za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Khimji na kukubaliana kendelea kukuza uwekezaji kati ya Tanzania na Oman.

Kupitia makubaliano hayo Tanzania na Oman zitakuwa na Mkataba wa Ushirikiano wa Kukuza Biashara na Uchumi (Comprehensive Economic Partnership Agreement -CEPA).

Akizungumza na Mhe. Khimji , Mhe. Chumi alieleza utayari wa Serikali ya Tanzania kushirikiana na mataifa hayo kwa maslahi ya nchi na wananchi wa pande hizo.

Mazungumzo hayo yamefanyika wakati wa Mkutano wa Nane wa Nchi za Bahari ya Hindi unaofanyika nchini Oman tarehe 16 na 17 Februari 2025 ambapo Mhe. Chumi anamwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news