ARUSHA-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma, amezindua rasmi mashindano ya mpira wa miguu ya Chuga Cup yaliyoandaliwa chini ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mheshimiwa Mrisho Gambo.
Mashindano hayo yanalenga kuhamasisha shughuli za michezo kwa vijana na kuwawezesha kujiendeleza kupitia soka.