TANGA-Wakazi wa Bongi, Handeni mkoani Tanga walikuwa wana shida ya maji iliyokuwa ikiwalazimu wanawake kutembea umbali wa kilomita tatu mpaka nne ili kufuata maji.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kama rais wa nchi na kama mama amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anawashusha wanawake ndoo kichwani na kusogeza huduma za maji karibia na maeneo yao.
Rais Samia hafanyi haya Handeni tu, bali amekuwa kinara wa kuhakikisha maeneo mbalimbali ya ndani ndani ya nchi yanafikiwa na huduma muhimu za kijamii.
Kwa kusogeza huduma ya maji karibu, Rais Samia amehakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama, wana muda zaidi wa kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii na hawahitaji kuweka maisha yao hatarini kwa ajili ya kupata huduma za msingi.