NCCR Mageuzi hakitaki ushirikiano uchaguzi mkuu ujao

DAR-Chama cha NCCR Mageuzi kimetangaza kutoshirikiana na chama chochote kile cha siasa kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 na kusisitiza kusimama wenyewe kuwapata wagombea wa nafasi kama Rais,wabunge na madiwani.
Chama hicho kimesema mwaka 2015 waliungana na umoja wa vyama vya upinzani UKAWA wakakubaliana baadhi ya majimbo waachiwe wakagombee, lakini chakushangaza CHADEMA na CUF walipeleka wawakilishi kwenye majimbo yao waliyokubaliana wawaachie kinyume na makubaliano yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 18,2025 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, Haji Ambar Khamis amesema kwamba, umoja huo hauna tija kwenye chama chao.

"Sisi tulipitia wakati mgumu sana ,tulikuwa na wagombea wanne wa nafasi ya ubunge,aliyepata ni nafasi moja tu ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia ,kitu ambacho walikosa nguvu kabisa nakupelekea kupoteza fedha kupitia umoja huo."

Amesema kwamba, kuna matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa siasa akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (CHADEMA) Tundu Lisu akisema kutoshiriki Uchaguzi Mkuu,hivyo hawatahusika na chochote na hawatakubaliana na kauli zake ama matamko anayotoa mara kwa mara kwani wanatambua tunu ya Taifa ya amani alioiacha Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.

Mwenyekiti huyo amezungumzia chaguzi za ndani za chama hicho zinazotarajiwa kufanyika Aprili 2025.

Amesema kupitia mkutano Mkuu utakofanyika Aprili wanatatangaza jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea urais kwa upande wa Zanzibar pamoja nakupitisha mabadiliko ya katiba ya chama hicho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news