TANZANIA imeendelea kushiriki na kuandaa mikutano ya Kimataifa kwa mara nyingine tena baada ya kupewa uenyeji wa mkutano wa kikanda wa mamlaka za viwanja vya ndege Afrika utakaofanyika jijini Arusha.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgaK-9QJ_x2KawBipBrQTOcS6-z1ynjLNuQSVIByBbNE8lKs9Uxass-CJ4awyGj1dE6A4IwjRuanjV8UvHmEtxjNPD7y50YsGPhEmc0LoMfzPN4wxwCi6nB06myMxlrYuzqkYMA9945iiFFY_a9DNGg0hvdMoUm69nVOUr4hiUJfvzhaPzVvuvUPNchFvh_/s16000/1001184660.jpg)
Tanzania imeendelea kupewa sifa hii ya kuandaa mkutano wa viwanja vyote vya ndege Afrika kwa kuangalia usalama wa abiria, huduma bora na usalama pamoja na idadi ya ndege zinazotua Tanzania na kuvipiku viwanja vingine vikubwa barani Afrika.
Katika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imekuwa ikiheshimika na kusikilizwa sana na mataifa ya Afrika na wakati mwingine kuchaguliwa kama eneo la kujadili masuala muhimu kama ya amani na upatanisho pamoja na mijadala mikubwa inayoamua mustakabali wa Bara la Afrika.
Kwa takribani wiki mbili za mwezi Januari na Februari ya mwaka 2025, Tanzania imeshiriki kuandaa mikutano miwili mikubwa ikiwemo mkutano wa Nishati pamoja na ule mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulio unganishwa na mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika Mashariki kujadili amani Masharriki ya Congo.
Kwa mikutano hii inaonyesha jukumu la Tanzania na umuhimu wake katika diplomasia na masuala ya kimataifa ikiwa ni njia mojawapo ya kuchechemua uchumi wa Taifa.
Tags
Habari