ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi anawakaribisha Wananchi wote katika uzinduzi wa Kampeni ya Sisi ni Wamoja #WeAreEqual inayosimamiwa na Taasisi ya Wake wa Marais wa Afrika(OAFLAD)

Wake wa Marais watashiriki akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Angeline Ndayubaha Ndayishimiye, Mke wa Rais wa Kenya Mama Rachel Ruto, wawakilishi kutoka Nigeria,Angola na Afisa Mtendaji Mkuu wa OAFLAD.
Aidha ,Tanzania itakuwa nchi ya 22 kati ya 54 kuzindua kampeni hii chini ya uwakilishi wa Mhe.Mama Mariam Mwinyi.