Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yakutana na ujumbe maalum kutoka Zambia



DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe maalum kutoka Tume ya Mishahara ya nchini Zambia leo Februari 21, 2025 katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Ushauri wa Kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Neema Ringo amesema,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inazikaribisha taasisi mbalimabli za ndani na nje ya nchi kuja kujifunza na kupata ushauri wa kisheria kutoka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
"Sisi tunajisikia fahari na heshima kutembelewa na Tume ya Mishahara kutoka Zambia, nichukua nafasi hii kuzikaribisha taasisi nyingine zije zipate huduma zetu."
Ujumbe huo kutoka nchini Zambia umeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Mishahara ya Zambia, Bw. Chembo Mbula ambae aliambatana na Mtendaji Mkuu wa TAZAMA nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news