PWANI-Jeshi la Polisi limesema video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kijana akikamatwa kwa nguvu ni tukio la ukamataji lililofanywa na Askari Polisi Februari 20,2025 katika eneo la Maili Moja Mkoa wa Pwani.

“Hata wakati anawakimbia Polisi walipojaribu kumkamata na kuwakimbia katika eneo la Mwendapole pikipiki aliyokuwa anandesha ilikuwa haina namba ya usajili, baadaye Polisi walipofanikiwa kumkamata katika eneo la Maili Moja ilikuwa haina namba ya usajili.
“Wakati wa ukamataji alianzisha vurugu ili kukaidi ukamataji pamoja na Askari Polisi kujitambulisha kwake, hata hivyo walifanikiwa kumkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Kibaha ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, ndugu zake nao wanazo taarifa kuwa anashikiliwa katika kituo hicho.”