Prince Karim Aga Khan IV afariki

LISBON-Kiongozi wa kiroho na Bilionea,Prince Karim Aga Khan IV amefariki dunia Februari 4, 2025 mjini Lisbon nchini Ureno akiwa na umri wa miaka 88.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa vikinukuu shirika lake la misaada, Aga Khan Development Network, The Aga Khan amefariki kwa amani, akiwa amezungukwa na familia yake.

Prince Karim Aga Khan IV ni kiongozi wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Ismaili Shia na mfalme wa Aga Khan ambaye ni mtaalamu wa maendeleo ya kijamii kote duniani. 

Alizaliwa Desemba 13, 1936 na alikuwa ni mtawala wa 49 wa familia ya Aga Khan, ambayo inahusiana na moja ya familia za kifalme za Ismaili. 

Prince Karim alikabidhiwa uongozi wa madhehebu ya Ismaili mwaka 1957, baada ya kifo cha babu yake, Aga Khan III.

Aga Khan IV amejitolea sana katika masuala ya elimu, afya na maendeleo ya jamii na alianzisha Aga Khan Development Network (AKDN), mtandao wa mashirika na miradi inayolenga kuboresha maisha ya watu hasa katika maeneo ya Afrika, Asia, na Mashariki ya Kati.

Vilevile anajulikana pia kwa kuchangia juhudi za kuleta amani na maendeleo kwa kutumia nguvu ya elimu na uongozi wa kiroho duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news