ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemjulia hali Mwanazuoni Maarufu Sheikh Ali Hemed Jabir Alfarsy (Maalim Aliyan)nyumbani kwake Mchangani Wilaya ya Mjini ,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Sheikh Aliyan ambaye ni Imamu Mkuu wa Masjid Maghfirah wa Mchangani pia aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),hivi karibuni alilazwa katika Hospital ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa na hatimaye kurejea Zanzibar na hali yake inaendelea vizuri.