ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Kamishna Mkuu Mpya wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA),Said Kiondo Athumani aliyemteuwa hivi karibuni.

Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla,viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,watendaji wakuu wa taasisi za umma na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama.