Rais Dkt.Mwinyi ana kwa ana na wafanyabiashara masokoni kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, atoa rai kwao

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa na upatikanaji wa bidhaa za vyakula na kuwataka wafanyabiashara kutopandisha bei wakati Ramadhani itakapoanza.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi, Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia mwenendo wa biashara na upatikanaji wa bidhaa za vyakula kuelekea Mwezi wa Ramadhani.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,Serikali inajipanga kwa ajili ya ujenzi wa masoko mengine maeneo mbalimbali ili kila mfanyabiashara afanye biashara kwenye mazingira rasmi.

Kuhusu suala la usafi wa masoko,Rais Dkt.Mwinyi ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia bora zaidi ya uhifadhi wa vidhaa za wafanyabiashara ili masoko kuwa safi wakati wote.

Amezielekeza taasisi zinazosimamia masoko hayo kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji na vipooza hewa katika masoko yote pamoja na kuimarisha usafi.
Ziara hiyo ya Rais Dkt.Mwinyi ni ya kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na ukarabati mkubwa wa Soko la Darajani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news