Rais Dkt.Mwinyi azindua boti za kubeba wagonjwa wakati wa dharura,asema huduma za afya hadi visiwa vidogo vidogo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kumaliza matatizo ya kiafya wanayokabiliana nayo wananchi wanaoishi katika visiwa vidogovidogo kwa kufikishwa katika matibabu kwa wakati ili kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika ikiwemo vya akinamama na watoto.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo baada ya kuzindua Boti za kubeba wagonjwa wakati wa dharura hafla iliofanyika Verde Mtoni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amefahamisha kuwa,boti hizo ni sehemu ya uimarishaji wa huduma za dharura na mfumo wa wa Rufaa kwa Wagonjwa wanaotoka kwenye visiwa wanaopewa Rufaa kutoka Vituo vya Afya kwenda Hospitali za Wilaya, Mkoa na Taifa.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imeamua kuzipeleka Boti hizo katika maeneo yenye changamoto kubwa zaidi na kwingine kutafanyiwa utaratibu wa haraka baadae.
Aidha, Dkt.Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kusaidia gharama za ununuzi wa Boti tano ambazo tatu tayari zimekamilika na mbili zitakamilika muda mfupi ujao.

Naye Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui amewahakikishia Wananchi wanaoishi katika Visiwa huduma za ihakika zitakazoanza hivi karibuni na kuwa tayari kuzitumia huduma hizo hususan akina Mama na watoto.
Boti hizo zimegharimu takribani shilingi bilioni 2 na zimetengenezwa na Kampuni ya QIRO GROUP LIMITED.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news