Rais Dkt.Mwinyi azindua Kituo cha Ukaguzi wa Vyombo vya Moto

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Uwekezaji wa Kituo cha Kisasa cha Ukaguzi na Upasishaji wa Vyombo vya Moto ni mapinduzi makubwa katika Sekta ya Usafiri hapa nchini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza katika ufunguzi wa kituo hicho Kwasilva kilichopo Dole Kizimbani Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kituo hicho ambacho ni ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Kizalendo ya Zenj General Mechandize kina uwezo wa kuhudumia vyombo vya moto takribani 300 kwa siku kwa kutumia mashine na Teknolojia ya Ukaguzi yenye Viwango vya Kimataifa.
Aidha,Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, kituo hicho ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya Sekta ya Usafiri na kitafungua ukurasa mpya wa usalama wa usafiri barabarani.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa, Serikali itaendelea kuthamini na kushirikiana na sekta binafsi kufanikisha miradi ya uwekezaji ya ndani na ile inayotoka nje ya nchi kwa mafanikio makubwa.

Akizungumzia usafiri wa umma, Dkt.Mwinyi amesema,Serikali imedhamiria kuwa na Usafiri wa Mabasi ya Kisasa ya Umeme yatakayotoa huduma bora kwa wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu ya mradi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Habiba Hassan amesema, mradi huo wa ubia baina ya Kampuni ya Zenj General Mechandise na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umegharimu shillingi bilioni 2.8 hadi kukamilika kwake na una uwezo wa kukagua vyombo vya moto 300 kwa siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news