TANGA-Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amebariki uwekezaji mkubwa wa Wizara ya Kilimo wa shamba la miwa Wilayani Pangani mkoani Tanga.

Amesema, Serikali inakwenda kuwekeza katika kilimo kikubwa cha miwa katika bonde la Pangani na kujenga viwanda vingi vya sukari ili kujitosheleza na bidhaa hiyo.
"Viwanda vingi vya sukari vilivyopo nchini vinazalisha sukari ya kawaida ya kula kuna sukari ya viwandani ambayo inaagizwa kwa wingi kutoka nje, sasa hili kuhifadhi na ku ‘save’fedha za kigeni tumeamua kikwanda hiki kijengwe ndani ya Tanga na kitajengwa Pangani, hatua hii ni kufungua fursa zaidi na kutengeneza ajira za wananchi,”amesema
“Barabara hii pia itakwenda kuchochea kwa wingi kilimo cha mihogo, nazi na kilimo kingine maeneo hayo na wakulima kuuza bidhaa zao nje ya Tanga,”amesema.
Mapema Mbunge wa Pangani ambaye ni Waziri wa Maji,Juma Aweso, amesema wamekuwa na mazungumza mazuri na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ya kutumia maji ya mto Pangani kufanya uwekezaji wa Kilimo kikubwa cha mashamba ya miwa hatua ambayo itasaidia vijana wengi kupata ajira.
“Tumezungumza na kaka yangu Waziri Bashe na ameahidi kufanya uwekezaji wa kilimo kikubwa cha miwa na vijana wetu kuweza kupata ajira,”amesema Aweso.