DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya wawili na uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uhamisho na uteuzi huo ni kama ifuatavyo:
-i.Mhe. Dkt. Vicent Naano Anney amehamishwa kutoka Wilaya ya Bunda kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa;
ii.Mhe. Aswege Enock Kaminyoge amehamishwa kutoka Wilaya ya Maswa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda;
iii.CPA Juma Ajuang Kimori ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO).
CPA Kimori anachukua nafasi ya Bw. Yona Killagane ambaye amemaliza muda wake;
iv.Prof.Edward Gamaya Hoseah ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Prof. Hoseah anachukua nafasi ya Dkt.Deo Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake;
V.Bi Renatha Mtunda Rugarabamu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Bi.Rugarabamu anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel Humba ambaye amemaliza muda wake;
Katika hatua nyingine, Jaji Mstaafu Awadh Mohammed Bawazir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA).
Jaji Mstaafu Bawazir anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Sauda Mjasiri ambaye amemaliza muda wake; na
vii.Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa Dkt.Salim Ahmed Salim kwa kipindi cha pili.