ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kumpangia kituo cha kazi Balozi.

Dkt. Amina Suleiman Msengwa ameteuliwa kuwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Msengwa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuucha Dar es Salaam.
Dkt. Msengwa anachukua nafasi ya Dkt. Albina Chuwa ambaye amemaliza muda wake;
Jaji Dkt. Ntemi Nimilwa Kilekamajenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Masoko na Mitaji.
Jaji Dkt. Kilekamajenga anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Deo John Nangela ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani;
Prof.Aurelia Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi yaBodi ya Kahawa. Prof. Kamuzora ameteuliwa kwa kipindi cha pili;
Bw. Abdulmajid Nsekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenziwa Bodi ya Chai Tanzania.
Bw. Nsekela anachukua nafasi ya Bw. Mustafa HamisUmande ambaye amemaliza muda wake;
Prof. Hozen Kahesi Mayaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Mipango yaMaendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Hozen ameteuliwa kwa kipindi cha pili; na
Balozi Dkt. Habib Galuss Kambanga amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda.