TANGA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kumpangia kituo cha kazi Balozi.

-(i) Dkt.Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango.
Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Msemwa alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments (WHI);
(ii) Prof. Philipo Lonati Sanga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).
Kabla ya uteuzi huu, Prof. Sanga alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Prof.Sanga anachukua nafasi ya Prof.Michael Ngumbi ambaye amemaliza muda wake;na
(iii) Balozi Susan Salome Kaganda amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uapisho wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.