Rais Dkt.Samia azindua Sera ya Elimu na Mafunzo mwaka 2014 toleo la 2023

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuwezesha na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera na Mitaala mipya ya Elimu ili ilete matokeo yaliyokusudiwa katika kuimarisha sekta ya elimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo Maalum kuhusu maono na mchango wake kwenye sekta ya Elimu kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Rais Dkt. Samia ametoa tamko hilo Februari 1,2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la Mwaka 2023 iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa Elimu kabla ya kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.

Rais Dkt. Samia amesema,mabadiliko na kukua kwa kasi kwa Teknoloji ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kunaweza kuwa na mchango chanya au hasi kutokana na namna jamii itakavyojipanga, hivyo ili kuendana na mabadiliko hayo ni lazima kutumia TEHAMA kutoa elimu kwa urahisi na kuwandaa vijana wetu kuwa na taaluma na ujuzi wa taaluma zinazoenda na mageuzi ya TEHAMA bila kuathiri maadili ya vijana hao.
Vile vile, Rais Dkt. Samia amesema Serikali haina budi kuwa na maandalizi ya kutosha kwa kuinua viwango vya ubora wa elimu, na kuwandaa vijana vizuri zaidi ili waweze kumudu stadi muhimu zitakazowawezesha kuajiriwa na kujiajiri pamoja na kuwajengea ujasiri na kuweza kujiamini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini bango maalum lenye ujumbe kuhusu Elimu mara baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya masuala ya Elimu katika viwanja vya ukumbi wa mikutano ya Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.

Rais Dkt. Samia pia amesema dhamira ya kufanya mabadiliko katika Sera ni kumuandaa kijana anayejiamini na mwenye nyenzo stahiki za kukabiliana na ushindani wa kikanda na kimataifa ili, kwa kutumia utajiri wa rasilimali zetu, aweze kunufaika kiuchumi.

Aidha,Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa kupitia Sera ya Elimu iliyoboreshwa, mwanafunzi amalizapo shule ya sekondari, atakuwa na ujuzi na stadi zitakazomuwezesha kutoa mchango kiuchumi kwa jamii inayomzunguka na taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda ya maonesho kuhusu masuala mbalimbali ya Elimu kabla ya kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Sera iliyoboreshwa pia italeta somo la ujasiriamali ambalo litakuwa la lazima kwa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne kwa lengo la kumuandaa mwanafunzi kupata misingi ya biashara, ili akiamua kujiajiri kwa kutumia stadi alizopata shuleni, aweze kufanya shughuli zake akiwa na maarifa ya biashara na apate manufaa zaidi.

Vilevile, ili kumuandaa kijana kushindana kikanda na kimataifa, wanafunzi watajifunza lugha mbalimbali za kimataifa ikiwemo kichina, kifaransa na kiarabu ambazo zitawapa umahiri wa lugha, watapata nyenzo muhimu ya mawasiliano na kuwawezesha kufanya biashara kikanda na kimataifa bila kikwazo cha lugha na zitawafungulia fursa mbalimbali zitokanazo na utandawazi.
Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia amesema,Serikali itapitia upya maslahi ya kada ya walimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kwa kuwa kada hiyo ndio msingi wa taalumazote, pamoja na kuendelea kuajiri walimu wenye sifa na kuwapa mafunzo stahiki iliwaendane na mwelekeo wa Sera mpya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news