Rais Dkt.Samia awasilisha Azimio la Dar es Salaam mbele ya CAHOSSCC jijini Addis Ababa

ADDIS ABABA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshirik ikatika kikao cha pembezoni cha Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSSCC), ambapo pamoja na mambo mengine amewashukuru Wakuu hao wa Nchi kwa kushiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati Afrika wa Misheni 300 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kuhusu masuala ya matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kwenye Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CAHOSSC Rais wa Kenya Mhe.William Ruto, Rais Dkt. Samia amewasilisha Azimio la Dar es Salaam na kueleza kuwa Afrika inapaswa kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi, kutetea maslahi ya Afrika na kuhahakisha inakuwa na mbinu mpya za kuteteana kutumia raslimali zake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akipokea Azimio hilo, Rais Ruto amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kufanikisha Mkutano wa Misheni 300 na Kikao kiliridhia Azimio hilo kuwasilishwa kwenye Baraza la Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupitishwa na Baraza hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kwa niaba ya Mwenyekiti wa AU, Rais wa Angola Mhe. João Lourenço katika ukumbi wa Nelson Mandela uliopo Makao Makuu ya Umoja huo, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025. Aidha, Tanzania imechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Umoja wa Afrika (Bureau of the African Union Assembly) kwa mwaka 2025.
Aidha, Baraza lilipitisha Azimio hilo bila kupingwa.Pia, Rais Dkt. Samia amepata fursa ya kuwasilisha Ajenda ya Nishati safi ya Kupikia iliyopendekezwa na Tanzania katika Baraza la Umoja wa Afrika ambapo ameeleza nishati hiyo safi ya kupikia ni hitaji muhimu kwa watu Milioni 900 barani Afrika ambao kwa sasa hawatumii nishati hiyo.

Baraza hilo limemtambua na kumpongeza Rais Dkt. Samia kama Kinara wa ajenda hii barani Afrika.

Awali,tarehe 15 Februari, 2025, Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikaliwa Umoja wa Afrika uliichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Umojawa Afrika (Bureua of the African Union Assembly) kwa mwaka 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC), Rais wa Kenya Mhe. William Ruto kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 16 Februari, 2025.

Kamati hiyo inaundwa na Angola kutoka Kanda ya Kusini (Mwenyekiti wa Umoja waAfrika 2025);Burundi kutoka Kanda ya Kati (Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti); Ghana kutoka Kanda ya Magharibi (Makamu wa Pili wa Mwenyekiti) na Tanzania kutoka Kanda ya Mashariki (Makamu wa Tatu wa Mwenyekiti).

Aidha, Mauritania iliyokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka 2024 kutoka Kanda ya Kaskazini itakuwa Katibu wa Kamati hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news