DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluahu Hassan amezindua Tume ya Rais ya Kutathmini kuhusu Masuala ya Mgogoro wa Ardhi katika Eneo la Hifadhiya Ngorongoro na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Uzinduzi wa tume hizo mbili umefanyika Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais Dkt. Samia tarehe 01 Disemba 2024 mkoani Arusha alipokukutana na kuzungumza na viongozi na wawakilishi wa wananchi wanaoshi eneo la Ngorongoro na maeneo jirani.

Aidha, tume hizo mbili zinajumuisha uwakilishi wa wananchi wanaoishi katika eneo la Ngorongoro na zinatarajia kufanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu.
Pamoja na mambo mengine, wakati wa uzinduzi wa Tume hizo mbili, Rais Dkt Samia ameeleza imani yake kuwa kazi itakayofanywa na Tume hizo itawezesha kupatikana kwa suluhu ya kudumu ya changamoto zilizowasilishwa kwake na viongozi na wawakilishi wa wananchi wanaoishi kwenye eneo la Ngorongoro.