OUAGADOUGOU-Serikali ya Jamhuri ya Burkina Faso imeidhinisha sheria mpya inayohusiana na wafungwa kushiriki katika shughuli za kilimo.
Rais Kapteni Ibrahim Traoré alitangaza kuwa, wafungwa na wanaosubiri kesi sasa wataruhusiwa kufanya kazi katika kilimo, na mfumo huo utasaidia katika kupunguza idadi ya wafungwa magerezani.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, wafungwa wataweza kutumia muda wao katika kilimo, na kama watafanya kazi kwa bidii, mwezi mmoja wa kazi utapunguza kifungo chao kwa miezi mitatu.
Pia,sheria hii inalenga kusaidia wafungwa kurekebisha tabia zao na pia kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi kupitia shughuli za kilimo.
Aidha,hii ni hatua muhimu ambayo inasaidia kuboresha hali ya wafungwa na pia kutoa mchango katika maendeleo ya kilimo nchini Burkina Faso.
Burkina Faso ni Taifa la Sahel lenye mapato ya chini na rasilimali ndogo za asili. Uchumi wake unategemea kilimo na madini, hasa uzalishaji wa dhahabu.
Aidha, katika Taifa hilo la Afrika Magharibi,zaidi ya asilimia 40 ya wakazi wake wanaishi chini ya mstari wa umaskini kitaifa.