DAR- Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb.) amempokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa ambaye amewasili nchini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025.