Samia Women Boxing Championship yafikia tamati

DAR-Mashindano ya Samia Women Boxing Championship yamefikia tamati siku ya leo tangu yalipoanza mnamo Januari 31, 2025 katika fukwe za Kawe jijini Dar es Salaam.
Katika fainali hizo mapambano nane yamefanyika huku pambano moja pekee likishandikina kufanyika kwa mpinzani wa Konsolata Laiza ambaye ni Fatuma Yazidu kushindwa kupanda ulingoni.

Kwenye pambano la kwanza Veronika Thomas kutoka makao makuu JKT amemtandika Leylat Kwa 'points'.

Pambano la pili Latifa Said kutoka JKT ameshinda Sarafina Fusi wa timu ya Ngome kwa 'points'.

Pambano la tatu Tatiana Ezekiel kutoka Gym ya Zugo amempiga Debora mwenda kutoka kwenye Gym ya Mzee Kinyogoli kwa 'points'.

Pambano la nne Vumilia Kalinga wa timu ya Ngome alimchakaza kwa 'points' Zawadi Amosi wa timu ya Makao Makuu JKT.

Pambano la tano Halima Vunjabei kutoka Maccoz Gym akapata ushindi wa 'TKO' dhidi ya Mariam Jonasi wa timu ya Balax kwenye raundi ya pili ya pambano la raundi tatu.

Pambano la sita Doricas Daud kutoka Gym ya Uwanja wa Kivita ameibuka kidedea kwa kumchapa Zulafa Iddi wa Gym ya Zugo kwa 'points'.

Pambano la saba Najima Isike wa timu ya Taifa ya ngumi alipata ushindi wa 'points' dhidi ya Joyce Saitabaru kutoka Polisi Arusha.

Pambano la nane Rachael Msingo kutoka Dodoma alimtandika Mariam Msabila kwa 'points' kutoka Gym ya Mzee Kinyogoli.

Mashindano hayo yalianza mnamo Januari 31, mwaka huu na kufikia tamati leo hii ambapo kwa siku zote tatu mapambano hayo yalifanyika kwa kuratibiwa na Shirikisho la Ngumi nchini Tanzania (BFT).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news