Serikali inaendelea kubuni mbinu kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu-Rais Dkt.Samia

TANGA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu huku akiiielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanuni za malipo ya kifuta jasho/machozi.
Ameyasema hayo leo Februari 24,2025 katika ziara alipokuwa akizungumza na wananchi Lushoto Mjini Mkoani Tanga.
"Tunaendelea kuongeza Askari Wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama wakali na waharibifu ikiwemo kutumia ndegenyuki (drones);" Rais Samia amesisitiza.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Naibu Waziri, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news